Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:15

Serikali ya Ethiopia imesema vikosi vyake vimekamata miji ya Dessie na Kombolcha

Mwanajeshi kutoka Jeshi la Ulinzi la Taifa la Ethiopia akionyesha ishara baada ya kumaliza mafunzo katika uwanja wa Dabat, Ethiopia, September 14, 2021.
Mwanajeshi kutoka Jeshi la Ulinzi la Taifa la Ethiopia akionyesha ishara baada ya kumaliza mafunzo katika uwanja wa Dabat, Ethiopia, September 14, 2021.

Serikali ya Ethiopia imesema vikosi vyake vimekamata tena miji ya Dessie na Kombolcha ikiwa ni ushindi wa karibuni wa eneo katika vita dhidi ya wapiganaji wa mkoa wa kaskazini wa Tigray.

Serikali ya Ethiopia imesema vikosi vyake vimekamata tena miji ya Dessie na Kombolcha ikiwa ni ushindi wa karibuni wa eneo katika vita dhidi ya wapiganaji wa mkoa wa kaskazini wa Tigray.

Vikosi vilivyokuwa pamoja na TPLF vilikuwa vimechukua udhibiti wa miji hiyo, katika mkoa wa Amhara zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kutishia kusonga mbele zaidi kuelekea mji mkuu wa Addis Ababa.

Waziri mkuu wa Ethiopia alitokea katika vituo vya televisheni vya ndani jumatatu, akitangaza kwamba vikosi vyake vilishinda vita dhidi ya vikosi kutoka Tigray. Abiy Ahmed alionekana katika mstari wa mbele akisema kuwa , ushindi utaendelea."tulisema Ethiopia haiwezi kushindwa kwa sababu tunawategemea nyinyi. maeneo mengi katika mkoa wa Amhara, ikiwemo Shewa ,Bati yote ambayo yako katika ukanda maalumu wa Kemise, Wello kwa kiasi Gondar kusini pamoja na Afar yote yameachiliwa. Tutaendelea hivyo hivyo kwenye maeneo yaliyobaki. Ushindi utaendelea. Hakuna kitu kitakachotuzuiya, adui atapigwa na wewe utashinda.” alisema.

XS
SM
MD
LG