Rais Mwai Kibaki alikubali uwamuzi wa Bw Kenyatta kujiuzulu kama waziri wa fedha na kumteua waziri wa masuala ya jiji la Nairobi Njeru Githae kuwa kaimu waziri wa fedha.
Katibu mkuu wa usalama wa Ndani Francis Kimemia ameteuliwa kuwa kaimu mkuu wa idara ya umaa akichukua nafasi ya Bw. Muthaura.
Tarifa iliyotolewa na ikulu ya Nairobi inaeleza kwamba Rais Kibaki amekubali uwamuzi wa kujiuzulu kwa wanasiasa hao wawili lakini Bw. Kenyatta anabaki na wadhifa wake wa naibu waziri mkuu.
Uwamuzi wa Bw Kenyatta na Bw Muthaura kuacha nafasi zao zinatokana na kishinikizo kutoka mshirika mkuu wa serikali ya mungano ya Kenya ya ODM kuwataka maafisa hao huondoka. Kishinikizo kinafuatia pia uwamuzi wa mahakama ya ICC kwamba, kuna ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi zao kuhusiana na tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu, kutokana na ghasia baada ya uchaguzi mkuu uliyopita nchini Kenya.