Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:13

Uhuru, Ruto na Sang watakata rufaa dhidi ya uwamuzi wa ICC


Watuhumiwa sita walofunguliwa mashtaka na mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Vita ICC.
(Juu kutoka kushoto): Maj. Gen. Mohammed Hussein Ali, ameachiliwa, Uhuru Muigai Kenyatta, and William Samoei Ruto;(Chini kutoka kushoto): Henry Kiprono Kosgey, aliyea
Watuhumiwa sita walofunguliwa mashtaka na mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Vita ICC. (Juu kutoka kushoto): Maj. Gen. Mohammed Hussein Ali, ameachiliwa, Uhuru Muigai Kenyatta, and William Samoei Ruto;(Chini kutoka kushoto): Henry Kiprono Kosgey, aliyea

Mara baada ya mahakama ya ICC kutangaza kwamba kunaushahidi wa kuendelea na kesi wa washtakiwa wanne, watatu walisema watakata rufaa.

Wakenya wengi wameridhika na uwamuzi wa Jumatatu wa mahakama ya kimataifa ya halifu wa vita, ICC, kwamba kuna ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi dhidi ya watu wanne kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kupanga na kuchochea ghasia baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Watatu kati ya watuhumiwa hao, waziri wa fedha, na makamu waziri mkuu Uhuru Kenyatta, waziri wa zamabi Willian Ruto na mwandishi habari Joshua Arap Sang, mara moja walitangaza kwamba watakata rufaa dhidi ya uwamuzi hao.

Hata hivo wachambuzi wa kisiasa wanasema watuhumiwa hao wanahisi wako juu kuliko sheria na kwamba hakuna kinaweza kufanyika bila ya kuhusika kwao.

Maur Bwanamwaka mchambuzi wa kisiasa mjini Mombasa anaema cha kusikitisha ni kwamba wanasiasa wa Kiafrika hawana uwezo wakuamua kujiuzulu wanapokumbwa na kashfa au matatizo yoyote ile.

XS
SM
MD
LG