Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:13

Wakenya wanne kupanda kizimbani ICC


William Ruto , Henry Kosgey na Joshua Arap Sang wakiwa katika kesi ya awali ICC
William Ruto , Henry Kosgey na Joshua Arap Sang wakiwa katika kesi ya awali ICC

Mahakama hiyo imefuta mashtaka dhidi ya mkuu wa polisi wa zamani Mohammed Hussein Ali na waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgey

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu – ICC imeamuru kuwa wakenya mashuhuri wanne wana kesi ya kujibu kwa kupanga na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu miaka minne iliyopita.

Mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague Jumatatu ilisema kwamba kuna ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi dhidi ya naibu waziri mkuu Uhuru Kenyata, waziri wa zamani wa elimu William Ruto, katibu wa bunge Fransic Muthaura na mkrugenzi wa radio Joshua Arap Sang.

Watatu kati ya washtakiwa nne, Uhuru, Ruto na Sang walitoa taarifa Jumatatu usiku kusema watakata rufaa, na wanaamini mahakama ya rufaa itafuta mashtaka yao.

Wote Kenyatta na Ruto walionesha azma ya kugombea katika uchaguzi mkuu wa Kenya unaotarajiwa mwaka huu. Ruto aliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kwamba bado ana azma hiyo.

Mahakama hiyo imefuta mashtaka dhidi ya mkuu wa polisi wa zamani Mohammed Hussein Ali na waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgey. Katika kesi zao majaji hawakuwa na ushahidi wa tuhuma zilizotolewa na waendesha mashtaka.

Kenya ilikumbwa na ghasia za kikabila baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2007. ghasia hizo ziliuwa takriban watu 1,300 na kukosesha makazi wengine zaidi ya laki tatu.

XS
SM
MD
LG