Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 17:55

Uganda yapata daraja jipya eneo la mto Nile

Rais Yoweri Museveni wa Uganda Jumatano amezindua Daraja jipya linalopita juu ya Mto Nile ambalo wataalamu wanasema litadumu kwa kipindi cha miaka 120 na litapunguza ajali.

Kufanikiwa kujengwa kwa daraja la Nile lenye kushikiliwa na nya za chuma lilijengwa kwa miaka minne iliyopita.

Daraja hilo Lina urefu wa mita 525 na limefadhiliwa kupitia mkopo wa serikali ya Japan kupitia Shirika la Ushirikiano la Kimataifa la Japan (JICA) na limegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 125,000,000.

Rais Museveni amesema daraja hilo jipya litatumiwa kupitisha magari na watembea kwa miguu ili kupunguza ajali. Amesema pikipiki zitapita katika daraja la zamani.


Picha zote kwa hisani ya Ofisi ya Habari ya Rais, Uganda.

Pandisha zaidi

Makundi

XS
SM
MD
LG