Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:48

Uganda na Tanzania vyanzo vikuu vya mapato ya utalii wa Kenya


Eneo la mbuga za wanyama la hifadhi ya Ol Pejeta, Kenya, Mei 2, 2020.AP Photo/Khalil Senosi)
Eneo la mbuga za wanyama la hifadhi ya Ol Pejeta, Kenya, Mei 2, 2020.AP Photo/Khalil Senosi)

Uganda na Tanzania zinaendelea kuwa chanzo kikuu cha soko la utalii nchini Kenya baada ya Marekani.

Kulingana na takwimu za karibuni zilizotolewa na Taasisi ya Utafiti ya Utalii, mwaka jana Kenya ilipokea watalii 870,465, idadi iliyoongezeka ikilinganishwa na ile ya 567,848 ya mwaka 2020.

Marekani ilikuwa chanzo cha juu cha soko hilo nchini Kenya ilikuwa na watalii 136,981, ikifuatiwa na watalii 80,067 kutoka Uganda, watalii 74,051 kutoka Tanzania na watalii 53,264 kutoka Uingereza na 42,159 kutoka India.

Sekta ya utalii Kenya imesajili ongezeko la asilimia 53.29 mwaka 2021, kufuatia kuondolewa kwa masharti ya COVID-19.

Kulikuwa na ongezeko la asilimia 34.76 la mapato ambapo liliingizia Kenya dola bilioni 1.46 ikilinganishwa na dola milioni 885 zilizoingia mwaka 2020.

Watu waliokuwa mapumzikoni ndiyo wengi waliowasili idadi yao ikiwa 299,802 ikiwa ni asilimia 34.44 ya wasafiri wote waliowasili nchini, wakifuatiwa na watu wanaozuru familia zao idadi yao ikiwa 257,357 (asilimia 29.57).

Wasafiri wafanyabiashara idadi yao ilikuwa 229,804, huku idadi ya wasafiri waliopitia viwanja vya ndege vya Kenya wakiwa ni 46,654 (asilimia 5.36).

Waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala alisema ujio wa wasafiri hao ulisukumwa na kufanyika kwa mashindano ya mbio za magari WRC’s Safari Rally na mashindano ya kimtaifa ya riadha ya vijana chini ya miaka 20 (World Athletics Under-20) nchini humo.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African

XS
SM
MD
LG