Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 10:14

Uganda Cranes yaichapa Stars 1-0


Wachezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania -Taifa Stars wameshindwa kutamba na kufungwa nyumbani mbele ya Uganda Cranes.
Wachezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania -Taifa Stars wameshindwa kutamba na kufungwa nyumbani mbele ya Uganda Cranes.

Timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes ) leo imefanikiwa kuishinda timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa bao 1-0 katika uwanja wa Mkapa, mjini Dar-es -salaam Tanzania .

Mchezo huo ni wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) itakayofanyika Algeria mwakani.

Timu ya taifa ya The Cranes ya Uganda walithibitisha kuwa na uwezo mkubwa na kupata ushindi ugenini na kufanikiwa kupata bao lao la kuongoza na la ushindi kunako dakika ya 88 lililowekwa kimiani na Travis Mutyaba.

Timu ya taifa ya Tanzania ilifanya mashambulizi kadhaa lakini ngome ya 'The Cranes' ilikuwa ni ngumu kupitika ikiongozwa na mabeki wake John Revita na Livingstone Mulondo.

Mara nyingi Taifa Stars imekuwa ikikutana na kigingi inapocheza Uganda Cranes kuwania kufuzu michuano ya kimataifa katika nbara la Agfrika na kwa maana hiyo Tanzania wana kazi kubwa ya kuhitaji ushindi katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Septemba 3, huko Uganda.

Uganda imefanikiwa kuingia katika michuano hii mara tano zilizopita 2011, 2014, 2016, 2018, and 2021.

Mara ya mwisho Taifa Stars kuifunga Uganda Cranes ilikuwa katika michuano ya kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika-AFCON 2019 ambapo Taifa Stars ilishinda kwa bao 3-0 katika uwanja wa Mkapa na timu zote mbili zilifanikiwa kuingia katika michuano hiyo ya Afrika iliyofanyika Cairo Misri.

Mshindi wa jumla baina ya timu hizi mbili atafuzu moja kwa moja Kwenda kwenye michuano ya CHAN itakayofanyika Algeria kuanzia Januari 13 hadi February 4, 2023.

Michuano ya CHAN inachezwa kati ya timu bora za kitaifa za bara la Afrika, ikishirikisha wachezaji wanaocheza katika ligi za ndani.

XS
SM
MD
LG