Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:40

Uchaguzi wa Rais Marekani wapamba moto


Donald trump
Donald trump

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanabashiri kuwa uwezekano wa uteuzi wake umeshuka kasi wakati wa- republican na wengine wakianza kuuliza maswali na kusema kuwa nafasi yake ya kushinda katika uchaguzi wa Novemba ni ndogo.

Mfanyabiashara maarufu wa nyumba Marekani, bilioniea Donald Trump analeta mvuto mpya kutokana na mtazamo wake wa suala la utoaji mimba , silaha za nyuklia za NATO, na pia jinsi anavyowachukulia wanawake wakati wapinzani wake wa kisiasa wakijaribu kuingilia uongozaji wake wa mstari wa mbele kama mgombea wa urais wa chama cha Republican.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanabashiri kuwa uwezekano wa uteuzi wake umeshuka kasi wakati wa- republican na wengine wakianza kuuliza maswali na kusema kuwa nafasi yake ya kushinda katika uchaguzi wa Novemba dhidi ya mpinzani wa democratic , waziri wa zamani wa mambo ya nje Hilary Clinton ni mdogo.

Hillary Clinton, Mgombea uteuzi wa Urais wa Democrat
Hillary Clinton, Mgombea uteuzi wa Urais wa Democrat

Katika siku za karibuni , vyombo vya habari vikubwa viliripoti kwamba anaweza kuwa mgombea asiyekuwa na mvuto mkubwa ambaye atashinda katika uteuzi wa chama huku utafiti wa kisiasa ukimwona kama atashindwa vibaya katika kinyang’anyiro cha mwisho cha kuziba nafasi ya rais Barack Obama atakapoondoka madarakani Januari mwaka ujao.

Trump ambaye hajawahi kuongoza ofisi yoyote ya kuteuliwa anauwezekano mkubwa kupata wajumbe wengi katika mkutano mkubwa wa Julai wa chama chake ambako chama kitateuwa mgombea wake kuwakilisha katika uchaguzi wa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG