Maafisa wa serikali wanasema wanaamini zaidi ya watu elfu 10 waliuwawa katika visiwa vya kati vya Leyte na Samar ambako kimbunga Haiyan kilifanya uharibifu mkubwa.
Kimbunga Haiyan cha sababisha uharibifu na maafa makubwa Ufilipino

1
Mama na watoto wake wanajificha nyuma ya jengo wakati kimbunga kikubwa cha Haiydan kina pita katika mji wa Cebu katikati ya Ufilipino, Nov. 8, 2013.

2
Mkazi mmoja anqatembea kando ya vifusi vya nyumba zilzioharibiwa na kimbunga kikubwa cha Haiyan katika mji wa Tacloban, jimbo la Leyte katikati ya Ufilipino.Nov. 9, 2013

3
Watu walonusurika wakitathmini uharibifu kutokana na kimbunga kikubwa cha Haiyan kilichoharibu mji wa Tacloban katikati ya Ufilipino, Nov. 9, 2013.

4
Picha kutoka hewani inayoonesha nyumba zilizoharibiwa kabisa kwenye mji wa pwani baada ya kimbunga kikubwa cha Haiyan kuharibu katikati ya Ufilipino. Nov. 9, 2013.