Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:27

Trump kupendekeza punguzo la misaada bajeti ya 2021


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump atapendekeza kupunguza msaada kwa nchi nyingine kwa mabilioni ya dola za Marekani katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021 wakati akitaka ongezeko la fedha katika kupambana na vitisho vya kiuchumi vya China na Rashia, afisa wa ngazi ya juu ameiambia Reuters.

Trump, ambaye ni Mrepublikan, alitaka katika pendekezo lake la bajeti mwaka 2019 kupunguza msaada kwa nchi nyingine lakini alikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka katika Bunge na ombi hilo halikufika mbali.

Bajeti yake ya hivi sasa anayopendekeza, ambayo itatolewa Jumatatu, ni muongozo wa pendekezo la matumizi ambalo siyo rahisi, kwa mara nyingine, kupitishwa, hususan katika mwaka huu wa uchaguzi.

Trump atataka kupunguza msaada kwa nchi nyingine kwa asilimia 21 katika pendekezo hilo, ambalo linataka dola bilioni 44.1 katika kipindi cha mwaka wa fedha unaokuja ukilinganisha na dola bilioni 55.7 zilizopitishwa katika mwaka wa fedha 2020, uongozi wa Trump umesema.

Msaada wa Ukraine utabakia katika kiwango kile kile cha 2020 katika pendekezo jipya. Trump alikutwa hana hatia wiki iliyopita kufuatia kesi iliyofunguliwa ikitaka kumuondoa madarakani kwa tuhuma za kuzuia msaada kwenda Ukraine akidaiwa kutaka Keiv imechunguze hasimu wake kisiasa Joe Biden, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratic na Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani.

XS
SM
MD
LG