Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:36

Baraza la Seneti kutoa uamuzi juu ya kesi ya Rais Trump Ijumaa


Maseneta wa Marekani wakimaliza siku ya mwisho ya maswali na majibu katika mchakato iwapo wamuondoe Rais Donald Trump madarakani siku ya Alhamisi.
Maseneta wa Marekani wakimaliza siku ya mwisho ya maswali na majibu katika mchakato iwapo wamuondoe Rais Donald Trump madarakani siku ya Alhamisi.

Kesi dhidi ya Rais Donald Trump kuhusu utumiaji mbaya wa madaraka na kuzuia Bunge kutekeleza kazi zake inafikia ukingoni Ijumaa pale Baraza la Seneti litakapokutana kuamua rais ana hatia au la.

Hoja ya Wademokrats kutaka kuletwa mashahidi ilionekana kushindwa baada ya Warepublikan waliotarajiwa kuungana nao kubadili mawazo yao na hivyo wachambuzi wanasema huenda kesi ikamalizika Ijumaa usiku na kumfutia mashtaka rais Trump.

Seneta Mrepublikan Lamar Alexander, aliyetarajiwa kuleta mabadiliko kwenye kesi hiyo, alitangaza jana kwamba hataunga mkono hoja ya kuruhusu mashahidi na kuvuruga matumaini ya Wademokrats kupata wenzao watatu tu kufikia kura 51 zinazohitajika kuruhusu mashahidi na kesi kuendelea.

Hivi sasa zinahitajika theluthi mbili za kura katika Baraza la Seneti kumuondoa rais jambo ambalo halitawezekana na hivyo kuna uwezekano mkubwa hatopatikana na hatia na kesi kumalizika.

Wachambuzi hivi sasa wanasema Wademokrats wanataka kuhakikisha kwamba Trump hatachukuwa uamuzi huu kuwa ni ushindi kwani wamedhihirisha alifanya makosa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG