Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:41

Trump atangaza pendekezo la sera mpya ya uhamiaji Marekani


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump anatangaza pendekezo lake la sera mpya ya uhamiaji, katika juhudi za kudhibiti aina ya watu wanaoingia hapa nchini.

Mpango huo una lengo la kuondoa utaratibu wa wahamiaji kuidhinishwa kutokana mahusiano ya kifamilia na mahitaji ya kibinadamu, na badala yake, kuangazia taaluma na ujuzi wa lugha..

Pendekezo hilo, linanuiwa kubadilisha malengo ya namna wahamiaji watakavyopatiwa vibali halali, likitoa kipaumbele kwa wenye ujuzi wa juu, na watu wasomi wenye ajira, au matarajio ya uwekezaji.

Trump anasema kuwa mpango huo utaimarisha usalama wa mpaka na kuunda mfumo utakaozingatia sifa za mtu, akisisitiza kwamba ni suala la ushindani wa uwezo wa mtu.

Pendekezo la Trump litaendelea kuweka idadi ya kadi za ukaazi halali Marekani maarufu Green Cards, zinazotolewa kwa takribani watu milioni 1.1 kila mwaka, lakini, iwapo sera hiyo itapitishwa itabadilisha malengo ya namna wahamiaji watakavyopatiwa ikitoa kipaumbele kwa wenye ujuzi wa juu na watu wasomi wenye ajira au matarajio ya uwekezaji badala ya mahusiano ya kifamilia kwa raia wa Marekani au mahitaji ya kibinadamu.

Kwa sasa asilimia 12 ya wahamiaji wanapewa ruhusa ya kuja Marekani kulingana na ujuzi wao na asilimia 66 kwa sababu ya uhusiano wao na familia ambazo tayari zipo Marekani kihalali.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG