Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:59

Trump asaini muswada wa $738 bilioni wa ujenzi wa kituo cha kijeshi cha angani


Rais Donald Trump (kulia) akimkabidhi Jenerali Jay Raymond, barua ya uteuzi wake kama mkuu wa operesheni za kijeshi za angani itakayoitwa U.S. Space Command, kwenye kituo cha jeshi la anga cha Andrews Air Force, Maryland, Disemba. 20, 2019.
Rais Donald Trump (kulia) akimkabidhi Jenerali Jay Raymond, barua ya uteuzi wake kama mkuu wa operesheni za kijeshi za angani itakayoitwa U.S. Space Command, kwenye kituo cha jeshi la anga cha Andrews Air Force, Maryland, Disemba. 20, 2019.

Rais Donald Trump amesaini Ijumaa sheria inayoruhusu kuundwa kwa kituo cha kijeshi cha angani na kuwapa wafanyakazi wa serikali kuu wiki 12 za likizo ya uzazi kwa wazazi wote wawili.

Baraza la Seneti linalodhibitiwa na Warepublikan limeidhinisha muswada wa sera ya ulinzi yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 738 baada ya Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na Wademokrat kupitisha uamuzi huo wiki iliyopita.

Hatua hiyo itawezesha kuanzishwa kwa kituo cha kijeshi cha angani kilichopendekezwa na Trump ikiwa ni tawi la sita la jeshi la Marekani ikiwa ni makubaliano ya Warepulikan kupitisha pendekezo la Wademokrat la livu ya uzazi, inayowapa wafanyakazi wa serikali kuu wiki 12 za likizo kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani.

Jenerali John "Jay" Raymond, kamanda wa Kituo cha Kijeshi cha Angani (Space Command) na Kituo cha jeshi la anga (Airforce Space Command) ameita tawi hilo jipya "ni muhimu kwa taifa," na kusema, "Uongozi wa Marekani katika anga za juu utawavutia wengine ulimwenguni. ...Tusifanye makosa. Marekani ni taifa bora duniani kwa masuala ya anga hivi sasa, na hivi leo tumepiga hatua zaidi.

Kikosi hicho cha angani kitakuwa ni tawi la kwanza la namna yake katika jeshi la Marekani kundwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 60 iliyopita.

Katika ngome ya kijeshi karibu na Washington, Trump alielezea anga za juu kama "eneo jipya la dunia la mapigano ya kivita".

XS
SM
MD
LG