Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 20:15

Honda yaboresha teknolojia ya robot


Ubunifu wa teknolojia ya kutumia ndizi kutoa sauti ya piano.

Maonyesho ya sayansi na teknolojia nchini Marekani maarufu kama STEM yaani sayansi teknolojia , uhandisi na mahesabu yamefanyika mjini Washington, DC nchini Marekani mwezi wa April 2018.

Maonyesho hayo yalishirikisha wanasayansi na wadau wa sayansi kutoka majimbo mbali mbali, taasisi binafsi, za kiserikali, na vyuo vikuu mbali mbali wakionyesha kazi mbalimbali za ubunifu .

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA anaripoti kuwa moja ya vivutio vikubwa ilikuwa ni Robot aliyetengenezwa na kampuni ya Honda na kupewa jina la Assimo.

Robot wa ajabu

Robot huyu kwa mujibu wa mratibu wa wahandisi wa kampuni ya Honda kutoka Marysville Ohio ametengenezwa akiwa na uwezo mkubwa wa kusikia , kukimbia kwa kasi, kuelewa maswali na kuweza kuwasiliana na binadamu kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.

Honda siku zote inatafuta njia mpya za ubunifu ili kusaidia watu katika maisha yao ili nao waweze kuchangia jamii zao.

Kampuni ya Honda ilifungua kitengo cha kushughulika na utengenezaji wa Robot zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Vipi Unicobb itasaidia walemavu

Kampuni ya Honda pia ilitangaza toleo la kifaa kiitwacho Unicobb ambayo itasaidia watu walsio na uwezo wa kutembea mwendo mrefu au wenye ulemavu wa miguu kuweza kuwasaidia kutoka sehemu moja au nyingine.

Kwa kutumia uzito na nguvu ya mwili wako bila kugusa au kusukuma kitu chochote mtu anaweza kusogea kutoka sehemu moja mpaka nyingine kwa kutumia kifaa hicho.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo kifaa hicho ni chepesi ambacho mtumiaji anakaa tu, lakini bado kinafanyiwa majaribio.

Kampuni ya Erector Engineering inawapa vijana na watoto nafasi kubwa ya kuwa wabunifu na katika banda lao wana vifaa mbali mbali vya kutengeneza robot au magari na watoto wanatumia uwezo wa ubunifui kutengeneza na kuchukua nyumbani.

Afisa wa kampuni hiyo Justin Olocruz ni afisa anasema: "Tunatumia vifaa halisi kwa hawa watoto kutengeneza vitu huku wakipata ujuzi wa kweli wa hali halisi ya mambo."

Mchango wa kampuni ya Explorlabs

Kampuni ya Explorlabs inafanya kazi ya kutambua chanzo cha ajali za moto kwani moto ni moja ya ajali zenye changamoto kutambua chanzo chake.

Wakiwa ni wachunguzi wa ajali hizo wanaonyesha jinsi ya kutambua, kufahamu na kufuatilia vyanzo vya ajali hizo.

Kelly Kenner, afisa wa kampuni ya ExplorLabs: “Ni kama kuanza kusoma na unakutana na ukurasa wa mwisho wa kitabu na ndio ulio nao. Kwa hiyo inabidi utumie ushahidi na njia za kisayansi kujua chanzo cha moto”.

Kampuni ya NASA

Nayo kampuni ya Lockheed Martin ikishirikiana na NASA inafanya safari za kwenda kwenye sayari ya Mars inayojulikana pia kama sayari nyekundu.

Kampuni hiiyo imejenga kwa kutumia kompyuta picha zinazofanana na chombo kinachokwenda Mars kutoka anga za juu kwa njia ya kompyuta.

Pia kulikuwa na ndege za kijeshi kutoka jeshi la anga la Marekani USAF –US Airforce ambazo zinafanya operesheni maeneo mbali mbali duniani ndege hizi zenye kasi ya hali ya juu na uwezo wa kubeba makombora ya angani na pia gharama yake ni dola milioni 143 , ina uwezo wa kuruka kwa sataili tofauti ikizuinguka hewani hata kuweka upande chini kwa juu ina uwezo mkubwa sana.

Chuo Kikuu cha Michigan

Hali kadhalika kulikuwa na vijana kutoka chuo kikuu cha Michigan ambao walionyesha jinsi wanavyoweza kusafirisha umeme kutoka mwilini mwa mtu kwenda kwenye chombo wakitumia app. iitwayo Mackey.

Mackey ikiunganishwa na kompyuta yenye piano na kuwekwa ndizi basi ndizi zile zinatoa mlio badala ya kompyuta hali kadhalika umeme huo unaweza kupitia kwenye mkono wa mtu na mkono huo ukatoa sauti ya piano.

Maonyesho haya ya kila mwaka lina lengo la kuinua vipaji na kuongeza hamasa ya kujifunza masomo ya sayansi kwa vijana nchini Marekani katika moja ya maeneo makubwa katiki jiji la Washington, DC kwenye Jengo la mikutano la Convention Center lenye ukubwa wa mita za mraba milioni 2.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Sunday Shomari, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG