Trump na Macron wamekiri kuwa wanashirikiana kuondoa tofauti zao katika mambo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa na Iran.
Trump amkirimu Macron kwa hafla ya chakula cha usiku
Marais hao katika hafla hii wanaonyesha urafiki wao kwa maneno na vitendo,

1
Rais Donald Trump, mkewe Melania Trump, Brigitte Macron, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuhudhuria hafla ya chakula cha usiku, White House, Washington, Aprili 24, 2018.

2
Maandalizi ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na White House kwa heshima ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Washington, Marekani, Aprili 23, 2018.

3
Rais Donald Trump na mkewe Melania na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte wakijiandaa kupiga picha ya pamoja katika ziara yao wakitembelea makazi ya Rais wa kwanza wa Marekani George Washington huko mji wa Mount Vernon, nje ya jimbo la Virginia.

4
Rais wa Marekani Donald Trump akiongea na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (watatu kulia kutoka chini) wakati alipokuwa akiongoza mkutano unaohusu mazungumzo zaidi baina ya ushirikiano wa pande mbili katika chumba cha mawaziri, ambao ulihudhuriwa na maafisa wengine baada ya ugeni huo kukaribishwa kwa hafla fupi huko White House.