Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 16:14

Tillerson afupisha ziara yake Afrika


Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini N'Djamena, Chad Machi 12, 2018.
Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini N'Djamena, Chad Machi 12, 2018.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amefupisha ziara yake ya Afrika kwa siku moja ili kurudi Marekani kushughulikia masuala muhimu likiwemo la Korea Kaskazini.

“Kutokana na umuhimu wa ratiba yake Waziri anarejea Marekani siku moja kabla ya kumaliza ziara yake, baada ya kumaliza mikutano ya kikazi huko Chad na Nigeria,” Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Steve Goldstein amesema Jumatatu.

Wakati Tillerson akiwa Afrika, Rais Donald Trump ametangaza kuwa amekubali mualiko wa Korea Kaskazini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un ifikapo May. Lakini hakuna mpango maalum uliokuwa umeandaliwa mpaka sasa .

Siku ya Jumatatu, Tillerson alitembelea N’Djamena, makao makuu ya Chad, kwa ajili ya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Idriss Deby.

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu anasafiri kuelekea makao makuu ya Nigeria, Abuja ili kukutana na Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari kabla ya kurejea Marekani.

Waziri Tillerson alishindwa kuhudhuria shughuli alizokuwa amepangiwa kuzifanya Jumamosi katika siku ya pili ya ziara yake nchini Kenya "kwa kuwa hajisikii vizuri", msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema.

Tillerson , miaka 65, yuko katika ziara yake ya kwanza ya kidiplomasia katika bara la Afrika, ambako tayari ametembelea Ethiopia, Djibouti, Kenya na Nigeria na Chad.

XS
SM
MD
LG