Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 20:42

Tillerson aendelea na ratiba yake Kenya


Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson akitoa hotuba ya kuwaenzi wahanga na majeruhi wa shambulizi la kigaidi nchini Kenya lililotokea mwaka 1998 katika ziara yake nchini Kenya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amerejea katika ratiba yake ya kawaida iliyoandaliwa katika ziara yake nchini Kenya Jumapili baada ya kusitisha shughuli zake Jumamosi kwa sababu alikuwa "hajisikii vizuri."

Tillerson aliweka shada la maua katika Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi Jumapili katika tafrija ya kuwaenzi wale waliouwawa na kujeruhiwa katika shambulizi la bomu kwenye ubalozi huo miaka 20 iliyopita.

"Ilivyokuwa nyote mnajua, mwaka 1998, magaidi walidhani wanaweza kutuvunja moyo na kutuangamiza watu wa Kenya na Marekani kwa kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Nairobi. Bila shaka walikuwa hawakosahihi. Miaka 20 baadae, tunakutana tena hapa kuwaenzi wale ambao walipoteza maisha yao na wale waliokuwa wamejeruhiwa," Tillerson aliwaambia wageni waliohudhuria wakiwemo watu walionusurika wakati wa shambulizi hilo.

Kati ya watu walionusurika ni Joash Okindo, ambaye anaendelea kufanya kazi katika Ubalozi wa Marekani baada ya kuvunjika mikuu katika mlipuko huo. Okindo, aliyekuwa amevaa medali ya ushujaa katika tafrija hiyo alikuwa ni mlinzi katika ubalozi huo siku ya shambulizi hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG