Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:01

Tanzania : Upinzani washinikiza uchaguzi kurudiwa


 Freeman Mbowe
Freeman Mbowe

Vyama vya upinzani nchini Tanzania bara na Zanzibar vimeitisha maandamano nchi nzima yasiyo na kikomo kupinga matokeo ya uchaguzi hadi hapo madai yao yatakapotekelezwa.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe alisema kilichofanyika si uchaguzi bali ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ZEC na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mbowe: “Katika kufikisha na kupaza sauti ya madai yetu, tunawatangazia wanachama wa vyama vyetu, wapenda demokrasia, watetezi wa haki za binadamu na wote wasiokubaliana na uchafuzi wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020 kushiriki katika maadamano ya amani yasiyo na kikomo kuanzia Jumatatu Novemba 2, 2020 hadi hapo madai yetu yatakapo tekelezwa.”

Upinzani pia umetoa orodha ya madai ambayo yanakubalika kati yao ikiwemo kurejewa kwa Uchaguzi Mkuu nchini humo. Pia wanataka Tume ya NEC na ZEC zivunjwe.

Vyama hivyo vya upinzani vikiwemo Chadema na ACT- Wazalendo vinapinga matokeo ya uchaguzi wa Jumatano ambapo rais aliye madarakani John Magufuli ametangazwa Ijumaa kuwa mshindi.

Wakati viongozi wa vyama hivyo wakiongea na waandishi wa habari Jumamosi wametoa wito kwa wananchi kuungana nao katika maandamano ya kudai uchaguzi kufanyika tena.

XS
SM
MD
LG