Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 16:26

Magufuli aongoza kwa kura nyingi katika matokeo ya awali


Dr John Pombe Magufuli

Rais wa Tanzania aliyeko madarakani John Pombe Magufuli siku ya Ijumaa anaongoza kufikia ushindi katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni.

Mapema Ijumaa, Magufuli alikuwa anaongoza kwa kura nyingi kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyo tangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakati Magufuli alitimiza umri wa miaka 61 Alhamisi, chama tawala, Chama Cha Mapinduzi(CCM) kilikuwa kinaongoza kwa ushindi mkubwa kulingana na matokeo ya awali yanayo onyesha ni wabunge wawili kutoka vyama vya upinzani walikuwa wamechaguliwa.

Lakini washirika wa Tanzania nchi za magharibi wametahadharisha kuwa madai ya wizi wa kura na vitisho yanaweza kupunguza nguvu ya ushindi wowote ule wa CCM.

“Kuwakamata viongozi wa upinzani siyo hatua ya serikali inayojiamini katika ushindi wake. Maalim Seif na wenzake ni lazima waachiwe mara moja,” Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald J Wright ameandika katika ujumbe wake wa Twitter.

Hamad alikamatwa Alhamisi kwa kuwataka wananchi kuchukua hatua dhidi ya kasoro za uchaguzi.

Serikali ya Marekani imesema vyama vya upinzani na makundi ya haki za kiraia walikuwa wametoa “malalamiko ya kweli” juu ya wizi wa kura na vitisho na idadi kubwa ya kura za ushindi za CCM zinapelekea kutilia mashaka ukweli wa hesabu hizo.

Dkt Wright amesema ni muhimu kwa Tanzania kuchunguza madai haya ya wizi wa kura kwa kurejesha uaminifu, kuondoa migawanyiko na kuheshimu utawala wa sheria.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG