Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 10:15

TANZANIA : Mwenyekiti wa bodi aeleza wasifu wa Ali Mufuruki aliyeaga dunia


Ali Mufuruki

Milionea wa Tanzania na mwenyekiti wa kampuni ya uwekezaji Infotech Investment Group, Ali Mufuruki, amefariki nchini Johannesburg, Afrika Kusini ambapo alikuwa anafanyiwa matibabu.

Mufuruki, ambaye ni mwanzilishi wa kikundi cha viongozi wa makampuni kijulikanacho kama CEO Roundtable of Tanzania (CEOrt) and kikundi kingine cha viongozi wa Afrika maarufu kama Africa Leadership Initiative (ALI) Afrika Mashariki, alifariki Jumamosi usiku, mwenyekiti wa (CEOrt) Sanjay Rughani amethibitisha hilo Jumapili.

“Wapenzi wajumbe wa bodi : Hii ni habari nisingependa kabisa kuwaletea lakini rafiki yetu kipenzi Ali Mufuruki amefariki usiku wa jan katika hospitali ya Morningside, Johannesburg Afrika Kusini….” Amesema Rughani katika ujumbe wake kwa wanachama wa CEOrt.

Ameeleza Mufuruki aliugua akiwa Dar es Salaam na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan Hospital. Baadae, alisafirishwa haraka kwenda Afrika Kusini Jumamosi mchana.

Mfanyabiashara na mtunzi, Mufuruki hadi hivi karibuni wakati wa uhai wake alikuwa mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania na kampuni ya Wananchi Group Holdings. Pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Mwananchi Communications Ltd, kampuni tanzu ya Nation Media Group. Pia alitumikia nafasi ya mdhamini wa chuo cha mafunzo ya maendeleo cha Mandela na ni mtunzi mwenza wa kitabu cha Tanzania Industrialisation Journey, 2016-2056.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG