Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 21:41

Ratiba ya Mazishi ya bilionea Mengi yatangazwa


Reginald Mengi Mwenyekiti wa IPP Tanzania

Mwanasheria wa familia ya marehemu bilionea na aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi, Michael Ngalo, Jumamosi ametoa ratiba ya mazishi.

Amesema mwili wa marehemu Mengi utawasilia saa 8:00 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Emirates.

Ratiba imeeleza kuwa baada ya hapo, mwili huo utapelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Siku hiyo ya Jumatatu na Jumanne utapelekwa kwenye viwanja vya Karimjee, Posta, jijini Dar kwa ajili ya kuagwa na wakazi wa Dar es Salaam na viunga vyake.

Baada ya kuagwa Karimjee, mwili huo utapelekwa nyumbani kwake, Ada-Estate, Kinondoni, jijini Dar na kesho yake Jumatano kusafirishwa kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kisha kijijini kwake, Nkuu, Machame, kwa mazishi yatakayofanyika kesho yake, Alhamisi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG