Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:55

Tanzania: Mahakama yatupilia mbali kesi ya Wamaasai dhidi ya serikali


Wanajamii wa Kimaasai nchini Kenya wakiandamana kupinga kuondolewa wa ndugu zao wa Kimaasai kutoka katika ardhi ya mababu zao nchini Tanzania, Kenya, June 17, 2022.
Wanajamii wa Kimaasai nchini Kenya wakiandamana kupinga kuondolewa wa ndugu zao wa Kimaasai kutoka katika ardhi ya mababu zao nchini Tanzania, Kenya, June 17, 2022.

Mahakama ya kikanda Ijumaa imetupilia mbali kesi iliyoletwa na kikundi cha wanakijiji wa jamii ya Kimaasai wakidai serikali ya Tanzania ilitumia nguvu kuwaondoa katika ardhi ya mababu zao iliyoko upande wa kaskazini mwa Tanzania.

Vikundi vya haki za binadamu vilisema uamuzi wa mahakama umepeleka ujumbe wa kutisha kuwa wenyeji ambao wanaweza kuondolewa katika makazi yao kwa madai ya kuhifadhi mazingira.

Serikali ilisema vijiji vinne ya Wamaasai viko ndani ya mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambayo hapo awali ilitengwa chini ya utawala wa kijeshi wa Uingereza kwa uwindaji lakini ikatengwa tena kwa ajili ya hifadhi ya mazingira na tawala zilizokuja baadae.

Mvutano wa umiliki wa ardhi kati ya wanakijiji wa jamii ya kimaasai na Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ulianza mwaka 2012 lakini baadae mwaka 2017 serikali iliagiza wakazi hao waondoke na majeshi ya usalama baadae yaliwaondoa kwa nguvu.

Mwaka 2018, Mahakama ya Kikanda ya Afrika Mashariki ilitoa amri ya muda kusitisha kuondolewa Wamaasai, hadi hukumu itakapotolewa.

Vikundi vya haki za binadamu na jamii za Wamaasai wanasema wanavijiji wako nje ya wigo wa hifadhi hiyo, na kuwa wanavijiji walikuwa waathirika wa kamatakamata ya mabavu iliyofanywa na polisi ikikusudia kuwaondoa kutoka katika ardhi yao ya asili ili kutoa fursa kwa watalii wanaowinda pembe na kudhibiti mazingira.

Siku ya Ijumaa, majaji watatu wa Mahakama ya Afrika Mashariki waliandika katika hukumu yao kuwa kesi hiyo haikuwa na hoja, wakisema Wamaasai hao walishindwa kuonyesha kuwa kuondolewa huko kulifanyika nje ya mipaka ya hifadhi hiyo.

Walisema sehemu kubwa ya ushahidi huo wa madai ya ukatili na utumiaji nguvuza kupitiliza ilikuwa uvumi na hauwafikiani.

Mwakilishi wa jamii ya Wamaasai alisema wanavijiji watakata rufaa.

“Hatujaridhishwa na uamuzi huu na tunaamini mahakama imefanya makosa katika kuchambua ushahidi tuliotoa,” alisema Jebra Kambole, aliyekuwa anawawakilisha Wamaasai katika hukumu hiyo ya mpito.

Fiore Longo kutoka taasisi ya Survival International, watetezi wa haki za wazawa, alisema hukumu ya mahakama ilikuwa ni pigo kwa Wamaasai na wazawa duniani kote.

Mahakama imetoa ishara tosha kwa jumuiya ya kimataifa kuwa ukandamizaji wa haki za binadamu na kuondolewa katika makazi dhidi ya wenyeji ni kitendo cha kuvumiliwa iwapo kinafanyika kwa minajili ya kulinda mazingira,” Longo alisema.

Tanzania imekuwa kwa muda mrefu ikikosolewa na jumuiya ya kimataifa kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya Wamaasai. Mwaka 2015, Bunge la Ulaya lilipitisha azimio kulaani serikali kwa kukiuka haki zao za kibinadamu.

Serikali ya Tanzania hata hivyo imekanusha kuwa imekiuka haki zao za kibinadamu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG