Maafisa wa Pakistani waliliambia shirika la habari la Associated Press Taliban ya Afghanistani ilifunga mpaka Jumapili kwa sababu Pakistan inadaiwa kuwazuia wagonjwa wa Afghanistan na wahudumu wao kuingia Pakistan bila hati za kusafiria.
Afisa wa mpaka wa Taliban Torkham, Mullah Mohammad Siddiq, aliwashauri raia wa Afghanistan kutosafiri kuelekea kwenye mpaka wa Torkham.
Alisema kupitia mtandao wa twitter kwamba Pakistan haikutimiza "nia yake ya dhati, lakini hakufafanua zaidi.
Taifa hilo lisilo na bahari, linashirikiana mpaka Pakistan wa takriban kilomita 2,600, wakati Torkham ni kituo kikuu cha usafiri kati ya nchi hizo mbili.
Facebook Forum