Chama cha wanahabari wa kujitegemea cha Afghanistan (AIJU), chenye makazi yake Kabul na kufanya uangalizi wa vyombo vya habari, kimetoa takwimu hizo Jumatatu katika maadhimisho ya siku ya Redio duniani.
Rais wa AIJU, Hujatullah Mujadidi, aliiambia VOA kwamba vituo vya redio 245 vilikuwa vikifanyakazi nchini humo kabla ya Taliban kuchukua utawala Agosti 2021, na kuajiri takriban watu 5,000, huku asilimia 25 wakiwa ni wanawake.
Lakini toka kipindi hicho vitu 117 vimesimamisha matangazo yake kutokana na matatizo ya kiuchumi.
Facebook Forum