Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:46

Mwanajeshi mmoja auwawa na raia 12 wajeruhiwa na mlipuko wa bomu Pakistan


Maafisa usalama wakichunguza mabaki ya gari katika eneo la mlipuko wa bomu, mjini Islamabad, Pakistani, Ijumaa, Desemba 23, 2022.AP
Maafisa usalama wakichunguza mabaki ya gari katika eneo la mlipuko wa bomu, mjini Islamabad, Pakistani, Ijumaa, Desemba 23, 2022.AP

Mlipuko wa bomu kusini magharibi mwa Pakistan Jumapili uliripotiwa kumuua mwanajeshi mmoja na kujeruhi watu 12, wakiwemo raia.

Shambulio hilo lililenga gari la kijeshi kwenye kituo cha ukaguzi wa usalama katika eneo la kati lenye ulinzi mkali la Quetta, mji mkuu wa jimbo la Baluchistan, wakaazi na maafisa walisema.

Si polisi wa jimbo au kitengo cha habari cha jeshi walotoa maelezo yoyote kuhusu majeruhi au sababu ya mlipuko wa Quetta. Kundi la waasi la Taliban la Pakistan, pia linaitwa Tehrik-i-Taliban Pakistan au TTP, lilidai kuhusika, likisema kwamba mmoja wa washambuliaji wake wa kujitoa mhanga ndiye aliyetekeleza shambulio hilo dhidi ya msafara wa kijeshi. Waasi hao walitoa idadi kubwa zaidi ya waathirika katika mlipuko huo lakini mara nyingi hutoa idadi kubwa katika mashambulio kama hayo.

Wafanyakazi wa uokoaji walithibitisha kuwa wapita njia watano walijeruhiwa katika shambulio hilo na kusafirishwa hadi hospitali ya kiraia iliyo karibu.

XS
SM
MD
LG