Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:50

Taiwan yaruhusu waandishi wa Marekani waliofukuzwa China kuendelea na uandishi kisiwani humo


Waziri wa Mambo ya Nje wa Taiwan Joseph Wu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Taiwan Joseph Wu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Taiwan Joseph Wu amewakaribisha waandishi watatu wa habari wa Marekani ambao vibali vyao vya kufanya kazi China vilifutwa, kuendelea na shughuli zao za uandishi katika kisiwa hicho.

Hatua ya Wo kuwakaribisha inafuatia tangazo la China mapema Jumamosi imewanyang’anya vitambulisho vya uandishi waandishi Wernau, Stu Woo na Stephanie Yang waliokuwa wanaandikia Jarida la The Wall Street.

Waandishi hao walionekana wakiwa na mkuu wa Jarida hilo ofisi ya China Jonathan Cheng uwanja wa ndege wa Beijing.

Wiki iliyopita, mamlaka nchini China iliwafukuza waandishi kadhaa waliokuwa wanafanya kazi na Jarida la The Wall Street, gazeti la Washington Post na gazeti la The New York Times

Pia iliamrisha Jarida la Time Magazine na kituo binafsi ya matangazo kinacho fadhiliwa na Marekani kinacho rusha matangazo ya Sauti ya Amerika watoe kwa mamlaka husika nchini China taarifa kamili juu ya shughuli wanazofanya nchini China.

China ilisema katika tamko lake Jumamosi kufukuzwa kwa waandishi hao ilikuwa ni kujibu hatua zilizochukuliwa kukataza chombo cha habari cha serikali ya China kufanya shughuli zake Marekani.

Hapo awali uongozi wa Trump ulivitaja vyombo vya habari vitano vya China vyenye ofisi zao Marekani kama balozi za kigeni na kuzuia idadi ya wafanyakazi wa China walioruhusiwa kufanya kazi kwa ajili yao, hatua iliyokusudia kuzuia ujasusi na ushawishi wa shughuli za Beijing nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG