Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:07

Tafiti Kenya yaonyesha Faru weusi, swala na wanyama wengine hatarini


FILE - Faru mweusi mwenye umri wa miaka katika hifadhi ya Wanyama ya Taifa Nairobi.(AP Photo/Sayyid Azim)
FILE - Faru mweusi mwenye umri wa miaka katika hifadhi ya Wanyama ya Taifa Nairobi.(AP Photo/Sayyid Azim)

Serikali ya Kenya inasema Faru weusi wa Kenya, swala aina ya Sable na wanyama wengine aina tatu wapo hatarini.

Pia wanyama aina tisa wakiwemo simba, tembo na duma wapo hatarini, serikali imesema.

Serikali imeeleza tishio hilo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, kwa mujibu wa shirika la habari la reuters.

Taifa hilo la Afrika Mashariki lilifanya uchunguzi wa miezi mitatu kwa wanyamapori, kuanzia Mei hadi Julai, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya zoezi kama hilo.

Tafiti hiyo ilikuwa na lengo la kuarifu sera zake za hifadhi.

Katika ripoti yake iliyotolewa Jumanne jioni, serikali ilisema juhudi za hifadhi zinakabiliwa na tishio, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu ambao wanajiingiza katika maeneo yaliyotengwa kwa wanyamapori.

Shughuli za kibinadamu kama kilimo, na ujenzi wa barabara na reli, zimeathiri usambazaji wa wanyama katika maeneo mengine, serikali ilisema.

XS
SM
MD
LG