Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 00:15

Hatimaye Tshisekedi ateua Waziri Mkuu DRC


Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga Ilukamba kuwa Waziri Mkuu, kwa mujibu wa tamko la Ikulu lililotangazwa na televisheni ya taifa Jumatatu.

Ilukamba anachukuwa nafasi ya Bruno Tshibala aliyetumikia nafasi ya waziri mkuu tangu April 7 mwaka 2007, chini ya utawala wa rais mstaafu Joseph Kabila.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters Ilukamba kabla ya uteuzi huu alikuwa Mkuu wa Kampuni ya Reli ya Taifa nchini Congo inayojulikana kama SNCC. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko.

Wakati huo huo, maelfu ya watu Jumatatu wamemlaki kwa shangwe na vigelegele Moise Katumbi, mpinzani mkuu wa Rais mstaafu Joseph Kabila, alipowasili leo kwenye uwanja wa ndege mjini Lubumbabshi, akirejea nyumbani kutoka uhamishoni.

Katumbi mwenye umri wa miaka 54, mwanasiasa pia mfanyabiashara alikuwa gavana wa jimbo la Katanga kwa muda mrefu. Katumbi alikataliwa kushiriki kwenye uchaguzi wa Disemba mwaka 2018, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 3 jela akiwa nje ya nchi.

Alikuwa anatuhumiwa kumiliki aridhi kinyume cha sheria, shutma ambazo alizikana. Lakini hukumu hiyo ilifutiliwa mbali na vyombo vya sheria vya DRC.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG