Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 00:18

Sudan yageuka uwanja wa vita, mitandao yenye maslahi yatumia mwanya huo


Mahasimu wa kivita mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdan Daglo, anayeongoza kikosi cha usaidizi wa haraka cha wanamgambo, RSF.
Mahasimu wa kivita mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdan Daglo, anayeongoza kikosi cha usaidizi wa haraka cha wanamgambo, RSF.

Sudan imekuwa ni uwanja wa vita wa majenerali hasimu wawili, lakini wanaungwa mkono na mitandao  ya washirika wa kimataifa ambao wanamaslahi ambayo yanaweza kuathiri mustakbali wa nchi hiyo, wachambuzi wanasema.

Makombora, mashambulizi ya anga na milio ya risasi yameendelea bila ya kusita mjini Khartoum tangu Jumamosi pale mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan akipigana vita na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, anayeongoza kikosi cha usaidizi wa haraka cha wanamgambo, RSF.

Zaidi ya watu 180 wameuawa na wengine 1,800 wamejeruhiwa, kulingana na UN, katika mapigano kati ya washirika wenza wa zamani na waasisi wa mapinduzi ya mwaka 2021.

Ikiwa na historia ya ndefu ya mapinduzi, taifa hilo la Afrika limekuwa likinufaika na eneo la kimkakati na kwa muda mrefu limekuwa likibembelezwa kwa ajili ya rasilmali zake za asili.

Russia na Umoja wa Falme za Kiarabu – pamoja na kutoa mabilioni kwa ajili ya bandari za Bahari ya Sham – zote zinashiriki katika eneo la Sudan linalodhibitiwa na RSF la uchimbaji wa dhahabu, kwa mujibu wa wataalam.

Kiwango kikubwa cha dhahabu ya nchi hiyo kimemfanya Daglo – maarufu kama Hemedti – tajiri, na katika mchakao huo amekuwa akiweka fedha kwa Kundi la Wagner, jeshi la mamluki la Russia, kulingana na Marekani, pamoja na UAE, soko kuu la dhahabu la Sudan.

Msaada wa Umoja wa Ulaya

Kikundi cha RSF cha Hemedti kilitokana na wanamgambo wa Janjaweed kilichoanzishwa na dikteta wa zamani Omar al-Bashir dhidi ya watu walio wachache wasiokuwa Waarabu katika mkoa wa magharibi wa Darfur kuanzia 2003, na kupelekea sshutuma za uhalifu wa vita.

Mchungaji ngamia aliyegeuka na kuwa kamanda mwenye nguvu katika eneo la magharibi mwa Sudan, ambalo lilikuwa ni kambi ya kupeleka wanajeshi wa RSF kwenye mapigano katika mzozo wa nchi jirani ya Libya, kulingana na wataalam.

Katika mahojiano ya televisheni mwaka mmoja baada ya mapinduzi ya 2021, Hemedti aliishukuru Italia kwa “kuendeleza mafunzo ya kiufundi” lakini alikanusha kuwa anapokea msaada wa Ulaya kuunga mkono uhamiaji usio wa kawaida kwa kuzuia njia za kuwawezesha wahamiaji kwenda Libya.

Magharibi mwa Sudan, ambako RSF pia ina maeneo yake katika mpaka wa Chad, bado “kuna silaha zimezagaa” kwa mujibu wa Reeves, ni muhimu kwa Hemedti, ambaye atajaribu “kutumia uhusiano wake na Chad na nguvu zake huko Darfur kupata silaha.”

Maslahi ya kina ya Misri

Kwa upande rasmi wa kidiplomasia, Burhan – kama mkuu wa nchi anayetambulika – anasifiwa kuwa ni muasisi wa kurejesha mahusiano ya kawaida na Israeli.

Jenerali huyo pia anamuangalia jirani wa Sudan ambao ni upande wa kaskazini Misri kwa msaada. Alisoma kwenye chuo cha kijeshi cha Misri pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, na Cairo ina maslahi kwa utulivu wa Sudan.

Nchi hizo mbili zina mahusiano makubwa ya kibiashara, wanashirikiana mpaka wenye urefu wa kilomita 1,200 (maili 745) na “wasi wasi wao unahusu usalama,” alisema Mirette Mabrouk, mfanyakazi mwandamizi wa Taasisi ya Mashariki ya Kati.

Msimamo wa Ethiopia

Hivi leo, jumuiya ya kimataifa -- ambayo tayari imekata misaada kwa Sudan kufuatia mapinduzi ya mwaka 2021 – inaonekana ina ushawishi mdogo ukilinganisha na nchi za kifrika na kiarabu.

Kuelekea katika mto Nile, Ethiopia, ambayo ni mwenyeji wa makao makuu ya Umoja wa Afrika nayo inashirikiana mpaka na Sudan, kuna uwezekano ikachukua muda wake.

Ikiwa tayari katika mivutano na Cairo juu ya mradi wa bwawa la Nile, “kitu cha mwisho wao (Addis Ababa) watataka kufanya ni kuwaudhi majenerali hao” ambao watakuwa ni sehemu ya mazungumzo ya mwisho, Reeves aliiambia AFP.

Vyanzo vya habari hii ni mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters

XS
SM
MD
LG