Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:24

Wasudan waliojaa hofu baada ya kukwama majumbani wajaribu kukimbia nje ya mji


Moshi ukisambaa angani baada ya shambulizi mjini Khartoum, Sudan, Jumapili, April 16, 2023.
Moshi ukisambaa angani baada ya shambulizi mjini Khartoum, Sudan, Jumapili, April 16, 2023.

Wasudan wenye hofu ambao  wamekwama ndani ya nyumba zao kwa siku kadhaa kutokana na mapigano katika mji mkuu Khartoum walikimbia Jumatano, na kubeba chochote walichoweza kuchukua huku wakijaribu kutoka nje ya mji.

Hatua hiyo imekuja baada ya suluhisho la kimaitaifa kusitisha mapigano kufeli na makundi hasimu yakiendelea kupigana katika mitaa kwa siku ya tano.

Kushindwa kuwepo kwa sitisho la mapigano kwa kipindi cha saa 24, licha ya shinikizo kutoka Marekani na mataifa ya kieneo, inaonyesha kuwa majenerali wawili wa juu wa Sudan wamedhamiria kupambana na ikiwezekana kwa kipindi kirefu kupigania udhibiti wa nchi.

Pia imesisitiza kukosekana uwezo wa jumuiya ya kimataifa kulazimisha ghasia hizo kusita, huku mamilioni ya watu wakiwa wamekwama ndani ya mapigano hayo.

Wakati milipuko na milio mizito ya risasi iliutikisa mji wa Khartoum, wakazi wa maeneo jirani kadhaa wameliambia shirika la habari la AP wameshuhudia mamia ya watu wakiwemo wanawake na watoto, wakikimbia kutoka kwenye nyumba zao, huku wakibeba mizigo, wengine wakitembea kwa miguu, wengine wakijazana katika magari.

Watu wakikimbia kutoka upande wa kusini ya Sudan Aprili 18, 2023, wakati mapigano kati ya jeshi na wanamgambo yakiendelea kwa siku ya nne. Picha na AFP).
Watu wakikimbia kutoka upande wa kusini ya Sudan Aprili 18, 2023, wakati mapigano kati ya jeshi na wanamgambo yakiendelea kwa siku ya nne. Picha na AFP).

Wakazi hao walikuwa wanahangaika huku chakula na mahitaji mengine ambayo yakiwaishia, wakitumaini kusimamishwa ghasia hizo katika milango yao – milio ya risasi, mabomu na mashambulizi ya anga, pamoja na wapiganaji wenye silaha wanaozunguka mitaani wakifanya wizi wa ngawira katika maduka na kuwashambulia wapita njia.

“Khartoum imegeuka kuwa mji wa shetani,” alisema Atiya Abdalla Atiya, katibu wa jumuiya ya Madaktari, ambaye bado yupo katika mji mkuu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG