Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 07:20

Sudan yaahidi kushirikiana na mahakama ya ICC


Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok

Kiongozi wa serikali ya mpito ya Sudan ameahidi kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC katika kesi yake dhidi ya kiongozi wa zamani nchini humo Omar al-Bashir.

Waziri Mkuu Abdalla Hamdok alikutana Jumapili na ujumbe kutoka ICC ukiongozwa na mwendesha mashtaka Fatou Bensouda.

ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa Bashir kwa tuhuma za mauaji ya halaiki, na uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na ghasia katika mkoa wa magharibi wa Darfur mwaka 2003.

Al-Bashir alijibu uasi wa Darfur dhidi ya utawala wake kwa kupeleka wanamgambo wa Janjaweed, ambao wanatuhumiwa kuua hadi watu laki tatu, na kuwafurusha makwao watu wapatao milioni 2.5.

Al-Bashir alipinduliwa na jeshi April mwaka 2019, kufuatia maandamano makubwa katika mji mkuu Khartoum na kwingineko ambayo yalianza Disemba mwaka 2018.

Hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka miwili jela nchini Sudan kwa tuhuma za ufisadi, na kwa sasa yuko kwenye kesi ya mapinduzi yam waka 1989 ambayo yalimwingiza madarakani.

XS
SM
MD
LG