Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:41

Fatou Bensouda wa ICC anaitembelea Sudan


Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama ya ICC
Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama ya ICC

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na mahakama hiyo tangu Omar al-Bashir alipoondolewa madarakani mwaka jana baada ya kufanyika maandamano makubwa yaliyokuwa yakipinga utawala wake

Ujumbe wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC unapanga kuitembelea Sudan kujadili kesi dhidi ya Rais aliyeondolewa madarakani Omar al-Bashir, na maafisa wengine wa zamani, serikali imesema Jumamosi.

Ujumbe huo unaongozwa na mwendesha mashtaka Fatou Bensouda, utajadili ushirikiano na Sudan juu ya watu wanaotafutwa bila kuwataja majina kulingana na taarifa hiyo. Ni ziara ya kwanza kufanywa na mahakama hiyo tangu Bashir alipoondolewa madarakani.

Bashir ambaye amewekwa jela huko Khartoum tangu alipoondolewa madarakani baada ya kufanyika maandamano makubwa mwaka jana anatafutwa na ICC kwa shutuma za uhalifu wa kivita, mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo lenye shida la mkoa wa Darfur nchini Sudan.

Mahakama hiyo yenye makao yake The Hague ilitoa hati ya kukamatwa kwa Bashir mwaka 2009 na 2010 ikimtuhumu kwa kusimamia mauaji katika kampeni yake ya kukomesha uasi katika mkoa wa Darfur.

XS
SM
MD
LG