Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 06:50

UN na serikali ya Sudan yasambaza misaada kwa waathirika wa mafuriko


Wakazi wakikusanya vifaa vyao baada ya mafuriko katika eneo la Al-Ikmayr, Omdurman, KhartoumSudan August 27, 2020. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Maafisa wa serikali ya Sudan na Umoja wa Mataifa wameanza kusambaza msaada wa dharura kwa maelfu ya watu walIopoteza makazi yao kutokana na mafuriko makubwa kuwasili kutokea mto Nile.

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema kwamba mafuriko hayo ambayo hayajawahi kushuhudiwa Sudan yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 na kuharibu maelfu ya makazi, na kuwalazimisha wakuu wa serikali kutangaza miezi mitatu ya hali ya dhaura.

Watu wengi hivi sasa wameweka kambi kando kando ya barabara na nyanda za juu ambako ni vigumu kuwafikia. Serikali ya Khartoum imesema Jumatano kwamba imetoa Zaidi ya dola milioni mbili laki saba kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo.

Shirika la wakimbizi la UNHCR limesema Jumatano kwamba kutokana na msaada wa Umoja wa Nchi za Kiarabu imeweza kusafirisha tani 100 ya vifaa vya dharura Ikiwa ni pamoja na mablanketi hadi majimbo 12 yaliyoathirika.

Karibu watu elfu 85 ambao hawakua na makazi na wakimbizi kabla ya mafuriko wameathirika na mafuriko mjini Khartoum, mashariki ya Sudan, kando ya mto White Nile na jimbo la Darfur.

Katika taarifa yake UNHCR imesema kunahitajika msaada wa dharura kwa haraka iwezekanavyo kutokana na uharibifu mkubwa uliotokea nchini humo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG