Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 20:23

Misri, Sudan zina wasiwasi juu ya kupungua kwa maji mto Nile


Bwawa la Ethiopia kama linavyoonekana katika picha ya satellite katika eneo la Mto Nile huko mkoa wa Benishangul-Gumuz, Ethiopia. MAXAR TECHNOLOGIES/ASSOCIATED PRESS
Bwawa la Ethiopia kama linavyoonekana katika picha ya satellite katika eneo la Mto Nile huko mkoa wa Benishangul-Gumuz, Ethiopia. MAXAR TECHNOLOGIES/ASSOCIATED PRESS

Sudan imesema Alhamisi kiwango cha maji katika mto Nile kimepungua wakati Ethiopia inaripotiwa kuanza kujaza maji katika bwawa lake la kuzalisha umeme la Grand Renaissance.

Misri nayo inataka taarifa rasmi kutoka kwa Ethiopia kuhusu hatua hiyo.

Sudan na Ethiopia zina wasiwasi kwamba hatua ya Ethiopia kujaza bwawa lake la kuzalisha umeme, itapunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha maji katika mto Nile.

Ethiopia inaona mradi wa kutengeneza umeme kwenye bwawa lake kuwa muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wake.

Waziri wa maji wa Ethiopia Seleshi Bekele, amethibitishwa kwamba bwawa hilo la umemee limeanza kujazwa maji.

Mazungumzo kati ya Ethiopia, Sudan na Misri, yalimalizika siku tatu zilizopita bila makubaliano.

XS
SM
MD
LG