Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 00:18

Sudan yatangaza sheria mpya kuimarisha haki za wanawake


Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok

Sudan imetangaza sheria za kuimarisha haki za wanawake, kupiga marufuku ukeketaji wa wasichana na wanawake na kuruhusu watu nchini humo kutumia pombe.

Wizara ya Sheria ya Sudan ilitangaza Jumamosi usiku kwamba watu nchini Sudan wasiokuwa Waislamu wataruhusiwa hivi sasa kutumia pombe, ikiwa ni uamuzi ambao unabadili sheria ya karibu miaka 40 iliyowekwa chini ya sera za Kiislamu wakati wa utawala wa rais wa zamani Jaafar al-Nimeiri.

Kulinganan na Umoja wa Mataifa asilimia 3 ya raia wa Sudan si Waislamu .

Utumiaji pombe ulipigwa marufuku kwa mara ya kwanza na Nimeiri mwaka 1993 kwa kutupa chupa za mvinyo wa whisky ndani ya mto nile katika mji mkuu wa Khartoum.

Serikali ya mpito ya Sudan halikadhalika inapiga marufuku ukeketaji wa wasichana na wanawake na mtu kubadili dini haitokuwa tena jambo la uhalifu.

Vile vile wanawake hawatakuwa na haja ya kuomba ruhsa kutoka kwa wanaume wa familia zao kuweza kusafiri na watoto wao.

Serikali ya mpito iliyochukuwa madaraka mwaka 2019 baada ya kupinduliwa rais wa muda mrefu Omar Al Bashir akiahidi kuifanya Sudan taifa la kidemokrasia na kukomesha ubaguzi na kufikia makubaliano na waasi wa taifa hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG