Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 16:10

Sudan : Waandamanaji waendelea na shinikizo la kumuondoa al-Bashir


Wanaharakati wanaopiga utawala wa Sudan wanasema vyombo vya usalama vimeuwa watu wasiopungua saba, akiwemo mwanajeshi, katika jaribio jingine la kuwaondoa waandamanaji waliokusanyika nje ya makao makuu ya jeshi, Khartoum, Aprili 9, 2019.

Waandamanaji nchini Sudan wanaendelea Jumatano kumtaka Rais Omar al-Bashir kuacha madaraka kwa kuamua kuendelea kuwepo mchana na usiku kwa siku ya tatu mfululizo nje ya makao makuu ya jeshi la nchi hiyo.

Maandamano hayo yalianza Disemba 19, 2019, kutokana na kupinga ongezeko la bei ya mikate na mafuta ya petroli na tangu hapo kuendelea hadi Jumatano wakishinikiza rais huyo ajiuzulu baada ya miaka 30 madarakani.

Waandamanji wamekuwa wakiitikia wito wa chama cha wanataaluma wa Sudan kufanya maandamano na kukaa nje ya makao makuu ya jeshi la nchi hiyo.

Naye mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Khartoum, Dama Moheideen anasema inaonekana hakuna kiongozi wa kweli wa vuguvugu hilo.

Walioshuhudia maandamano hayo wamesema majaribio ya baadhi ya askari kuwaondoa waandamanji hao yaliwasababisha wanajeshi kuwalinda hao waandamanaji.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG