Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:00

Maandamano Sudan : Gesi ya kutoa machozi yaua raia


Waandamanaji nchini Sudan wakipinga utawala wa Omar al-Bashir huko mjini Khartoum, Feb. 14, 2019.
Waandamanaji nchini Sudan wakipinga utawala wa Omar al-Bashir huko mjini Khartoum, Feb. 14, 2019.

Muuzaji matunda, raia wa Sudan, amefariki mjini Khartoum, baada ya kuvuta gesi ya kutoa machozi iliyotumika na maafisa wa usalama kuwatawanya waandamanaji.

Maafisa wa afya, na familia ya marehemu, wamesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 62, mkazi wa Bhari, mtaa ulio kaskazini mwa Khartoum, alikufa akipokea matibabu hospitalini.

Gesi ya kutoa machozi ilirushiwa waandamanaji waliokuwa wakiandamana barabarani jana jumapili.

Maandamano ya Sudan, yalianza Desemba 19, 2018, wakati serikali ilipandisha bei ya mkate.

Tangu wakati huo, maandamano yameendelea na kumekuwepo mapambano kati ya polisi wa kuzuia ghasia na waandamanaji.

Maandamano sasa yamegeuka na kuwa ya kutaka rais Omar Al-Bashir kuondoka madarakani.

Serikali ya Sudan inasema watu 31 wamekufa kufuatia maandamano hayo, lakini wachunguzi wa kimataifa wa haki za binadamu wanasema hadi sasa watu 51 wameuawa.

Sudan inapanga kuandaa uchaguzi mkuu mwaka ujao 2020, na rais wa sasa Omar Al-Bashir ambaye ametawala nchi hiyo tangu mwaka 1993, baada ya mapinduzi ya kijeshi, ametangaza kuwania mhula wa tatu.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG