Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 06:43

Waandamanaji huko Sudan wanataka Bashir aondoke madarakani


Rais wa Sudan, Omar al-Bashir
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir

Waandamanaji wanaripotiwa kulenga na kuzichoma ofisi za chama cha Bashir na walitoa wito wa kumalizika utawala wake wa miaka 29. Bashir aliingia madarakani katika mapinduzi ya jeshi mwaka 1989

Polisi wa kupambana na ghasia walifyatua gesi ya kutoa machozi kwa maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu wa Sudan siku ya Jumapili wakati wa maandamano yanayotoa wito kwa Rais Omar Al Bashir kujiuzulu yakiendelea kwa wiki ya tatu.

Umati wa waandamanaji walikusanyika mjini Khartoum ukitekelezea wito wa muungano wa wasomi nchini Sudan kundi linalojumuisha madaktari, waalimu na wahandisi ambalo limeitisha migomo na maandamano tangu Disemba mwaka jana. Polisi walijibu tukio kwa kufyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji. Video iliyochapishwa kwenye mtandao kutoka kwa wanaharakati wanaopinga serikali inaonesha watu wakikimbia pembeni ya mitaa na njia za vichochoroni kuepuka gesi hiyo.

Waandamanaji huko Sudan wakitaka Rais Bashir aondoke madarakani
Waandamanaji huko Sudan wakitaka Rais Bashir aondoke madarakani

Serikali ya Sudan ilisema watu 19 waliuwawa wakiwemo wafanyakazi wawili wa usalama tangu maandamano yalipoanza kaskazini-mashariki ya mji wa Atbara hiyo Disemba 19 mwaka 2018. Wakati huo huo kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilieleza watu 37 wameuwawa katika ghasia hizo.

Maafisa wamefunga shule na kutangaza amri ya kutotoka nje na hali ya dharura nchini humo katika maeneo kadhaa tangu ghasia zilipoanza. Waandamanaji wanaripotiwa kulenga na kuzichoma ofisi za chama cha Bashir na walitoa wito wa kumalizika utawala wake wa miaka 29. Bashir aliingia madarakani katika mapinduzi ya jeshi mwaka 1989.

XS
SM
MD
LG