Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 02, 2023 Local time: 18:20

Sudan : Omar al-Bashir afikishwa mahakamani


Omar al-Bashir akiwa mahakamani nchini Sudan

Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir aliyepiduliwa Aprili 2019, amefikishwa mahakamani Jumatatu ili kuanza kusikiliza kesi za ufisadi dhidi yake.

Bashir aliyetumikia nafasi ya urais kwa miaka 30 anakabiliwa na tuhuma za kuhifadhi fedha za kigeni kinyume cha sheria pamoja na kupokea zawadi kinyume cha sheria.

Bashir amewaambia wachunguzi kwamba alipokea mamilioni ya dola taslimu kutoka Saudi Arabia kulingana na mpelelezi aliyetoa ushahidi mbele ya mahakama.

Kiongozi huyo wa wazamani akiwa amevalia kanzu ya kiutamaduni wa Sudan alionekana akifuatilia keshi hiyo wakati akiwa kwenye sehemu aliyotengewa ndani ya ukumbi wa mahakama.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuwa kesi inayoendelea dhidi ya Bashir isiwe kigezo cha kutofikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC anakokabiliwa na mashitaka ya uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu pamoja na mauaji ya halaiki wakati wa vita vya Darfur nchini humo.

Mwezi Mei, Bashir alifunguliwa mashtaka ya kuchochea na kujihusisha na mauaji ya waandamanaji ambao walipinga utawala wake.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG