Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 02:57

Jeshi na Raia : Makubaliano ya kihistoria yafikiwa Sudan


Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, Naibu mkuu wa baraza la kijeshi, kulia, na kiongozi wa waandamanaji nchini Sudan Ahmed Rabie baada ya kutia saini mkataba wa kihistoria wa makubaliano mjini Khartoum, Sudan, Agosti 4, 2019.
Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, Naibu mkuu wa baraza la kijeshi, kulia, na kiongozi wa waandamanaji nchini Sudan Ahmed Rabie baada ya kutia saini mkataba wa kihistoria wa makubaliano mjini Khartoum, Sudan, Agosti 4, 2019.

Wajumbe wa muungano wa upinzani wa Sudan na wale wa baraza tawala la kijeshi wametia saini makubaliano ya kihistoria ya kushirikiana madaraka, mjini Khartoum Jumamosi.

Makubaliano hayo yanafunguwa njia kwa pande hizo mbili kuunda serikali ya mpito kati ya wanajeshi na raia itakayoongoza Sudan kwa miaka mitatu.

Sherehe za kutia saini mkataba zilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Ethopia Abiy Ahmed na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini pamoja na maafisa kutoka nchi jirani na mabalozi wa kimataifa.

Makubaliano ya kuunda kipindi cha mpito yamefikiwa baada ya miezi kadhaa ya maandamano yaliyozuka mwezi Disemba 2018 kutokana na kupanda bei za mafuta na mkate na hatimaye kugeuka na kumtaka kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir kuachia madaraka.

Jeshi lilimuondosha Bashir kwa nguvu mwezi April 2019, lakini waandamanaji waliendelea na malalamiko yao wakitaka kuundwa kwa utawala wa kidemokrasia na jeshi kuachia madaraka baada ya miaka 30 ya utawala wa kimabavu wa Bashir.

Baraza la mpito la kijeshi TMC, liliokuwa madarakani tangu mwezi April baada ya kumondowa Bashir limekuwa likijadiliana na mungano mkuu wa upinzani na waandamanaji , Forces of Freedom and Change (FFC) kupitia upatanoishi wa Umoja wa Afrika, kuweza kufikia makubaliano hayo.

Chini ya makublaino hayo yaliyoidhinishwa siku ya Jumamosi waziri mkuu anatarajiwa kutajwa ifikapo Jumanne Ogusti 20, na siku nane baadae baraza la mawaziri litatangazwa. Jeshi litaendelea kushikilia mamlaka ya nchi kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya utawala wa wananchi kuchukua mamlaka kamili.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG