Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:59

Marekani inaupongeza mkataba wa kushirikiana madaraka Sudan


Nembo ya wizara ya mambo ya nje Marekani
Nembo ya wizara ya mambo ya nje Marekani

Wizara ya mambo ya nje Marekani imetoa wito wa kukuza kile inachokiita baraza la uhuru lenye mzunguko wa madaraka kwa nafasi ya rais kutoka upande wa jeshi na kiraia kwa miaka mitatu

Marekani inasema inaukaribisha mkataba wa kushirikiana madaraka uliobuniwa kumaliza miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa nchini Sudan.

Mkataba huo uliafikiwa ijumaa kati ya viongozi wanaoandaa maandamano na majenerali wanaotawala nchi baada ya kufanyika mazungumzo ya siku mbili. Marekani imetoa wito wa kukuza kile inachokiita baraza la uhuru lenye mzunguko wa nafasi ya rais kutoka upande wa jeshi na kiraia kwa miaka mitatu.

Wizara ya mambo ya nje Marekani ilisema hii ni hatua muhimu kusonga mbele. Ilielezea matumaini kwamba mkataba utaongoza kuundwa kwa serikali ya muda inayoongozwa kiraia ambayo ndio inasisitizwa na watu wa Sudan.

Waandamanaji Sudan wanaosisitiza jeshi likabidhi utawala kwa raia
Waandamanaji Sudan wanaosisitiza jeshi likabidhi utawala kwa raia

Nchi ya Sudan imeingia kwenye matatizo ya kisiasa tangu majenerali walipomuondoa Rais wa muda mrefu Omar Al-Bashir kwa njia ya mapinduzi mwezi April kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya umma nchi nzima.

XS
SM
MD
LG