Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 04:25

Umoja wa Mataifa unawaondoa baadhi ya wafanyakazi wake Sudan


Baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Sudan

Hata hivyo msemaji wa Umoja wa Mataifa hakutoa taarifa zaidi juu ya wafanyakazi wangapi walikuwa wanaondolewa, mahala gani walikuwa wanapelekwa, lini watarejea tena kuendelea na kazi na ni wafanyakazi wangapi wataendelea kubaki nchini Sudan

Umoja wa Mataifa ulieleza Jumatano unawaondoa kwa muda baadhi ya wafanyakazi wa kiraia kutoka Sudan kwa sababu ya hali ya usalama nchini humo mahala ambako wanajeshi siku ya jumatatu waliwashambulia waandamanaji walioweka kambi nje ya makao makuu ya jeshi na kusababisha vifo vya waandamanaji.

Upinzani wenye uhusiano na wahudumu wa afya ulieleza idadi ya vifo kutoka operesheni ya Jumatatu na kukamatwa kiholela imeongezeka kufikia watu 108 na kwamba idadi ilitarajiwa kuongezeka zaidi. Hakuna idadi rasmi ya waliofariki au kujeruhiwa iliyotolewa.

Shambulizi hilo linafuatia wiki kadhaa za mvutano kati ya baraza la jeshi linalotawala na makundi ya upinzani pamoja na waandamanaji kuhusu nani anatakiwa kuongoza serikali ya mpito ya Sudan kuelekea demokrasia na imekuwa mojawapo ya mlipuko mbaya wa ghasia tangu jeshi lilipomuondoa madarakani Rais Omar al-bashir mwezi April baada ya miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya utawala wake wa miaka 30.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan, Farhan Haq alieleza kwamba kile wanachofanya ni kuwahamisha kwa muda baadhi ya wafanyakazi kutoka Sudan. Anasema bado watakuwepo wafanyakazi kadhaa wa kufanya operesheni muhimu lakini kwa sababu ya usalama inabidi baadhi yao waondolewe.

Hata hivyo msemaji huyo hakutoa taarifa zaidi juu ya wafanyakazi wangapi walikuwa wanaondolewa, mahala gani walikuwa wanapelekwa, lini watarejea tena kuendelea na kazi na ni wafanyakazi wangapi wataendelea kubaki nchini humo.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan

Aliongeza kusema kuwa wafanyakazi wanaohamishwa walikuwa ni maafisa wa kiraia na hakuna wanajeshi wa usalama wanaoondolewa.

Kulingana na ukurasa wa tovuti wa Umoja wa Mataifa kazi za umoja huo nchini Sudan zinajumuisha ushirikiano wa maendeleo na msaada wa dharura pamoja na operesheni za walinda amani zinazofanywa na jeshi la pamoja la Umoja wa Afrika na operesheni ya Umoja wa Mataifa-UNAMID huko Darfur iliyokuwepo tangu mwaka 2007.

XS
SM
MD
LG