Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 04:03

Somalia yaishutumu Kenya ina 'njama za kuiyumbisha'


FILE - Wanajeshi wa Kenya wakitoa heshima zao za mwisho kwa wanajeshi wa Kenya waliouawa Somalia katika kambi ya Eldoret, Kenya Jumatano, Januari 27, 2016.
FILE - Wanajeshi wa Kenya wakitoa heshima zao za mwisho kwa wanajeshi wa Kenya waliouawa Somalia katika kambi ya Eldoret, Kenya Jumatano, Januari 27, 2016.

Waziri wa habari wa Somalia Osman Abukar Dubble ameishutumu Kenya kwa kupanga kusababisha vurugu Somalia wakati ikijiandaa na uchaguzi wa ubunge na urais, televisheni ya taifa ya Somalia imeripoti.

Waziri huyo ameishutumu Kenya kuiingilia kisiasa na kuhifadhi viongozi wa upinzani nchini mwake.

Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya imekanusha ripoti kwamba inaingilia masuala ya ndani na siasa za Somalia.

Madai zaidi ya Somalia ni kuwa wanasiasa kutoka jimbo la kusini la Juballand ni miongni mwa wale ambao awali walifanya mikutano mjini Nairobi na majadiliano kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Somalia wa mwaka.

Dubble anasema “ Mogadishu haijawahi kumpatia hifadhi mwanasiasa yoyote wa upinzani kutoka Kenya, ambaye anataka kusababisha mivutano kwa majirani zetu.

Lakini badala yake Nairobi imekuwa kituo ambacho mashambulizi dhidi ya Somalia yanafanyika.

Waziri huyo wa Habari anasema Nairobi imekuwa kituo ambacho makubaliano yanayofikiwa ndani ya Somalia yanakiukwa.

Na kwamba Nairobi imekuwa pia mahala ambapo mipango ya kusababisha mizozo ya kisiasa yenye lengo la kuleta vurugu inafanyika dhidi ya serikali yetu.

Ndio maana tumemwondoa balozi wetu kutoka Nairobi kwa ajili ya mashauriano , alisema hayo waziri wa habari.”

XS
SM
MD
LG