Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 03:56

Maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Somalia yaendelea


Maafisa wa usalama nchini Somalia wakati wa uchaguzi wa mwaka 2017

Somalia imeanza kutoa mafunzo kwa maafisa wa kushughulikia malalamiko yatakayojitokeza katika uchaguzi mkuu ujao, licha ya wagombea wa urais kutoka vyama vya upinzani kuwashutumu maafisa hao kwa kuwa na upendeleo.

Wanasiasa wa upinzani wanasema kwamba wengi wa maafisa hao ni wafuasi wa rais Mohamed Abdullahi Farmaajo.

Wagombea 12 wa urais na wawakilishi wa vyama vyao wanafanya mazungumzo katika mji mkuu wa Mogadishu.

Mazungumzo hayo yanahusu umoja na usimamizi mzuri wa uchaguzi mkuu ujao.

Abdirahman Abdishakur ni mmoja wa wagombea wa urais anayehudhuria mkutano huo.

“Uchaguzi ni shughuli ngumu sana kwa taifa lenye misukosuko kama Somalia. Kwa hivyo, tumekuja Pamoja kujadiliana kuhusu swala hilo. Tumekuwa tukishirikiana n ajamii kwa siku tatu zimepita. Tumekuwa tukiwajumulisha viongozi wa koo, watu wa kawaida, wafanyabiashara na vijana. Tunajaribu kushirikiana katika kukubaliana namna ya kuendesha uchaguzi mkuu na jinsi ya kushughulikia migogoro endapo itajitokeza baada ya uchaguzi.”

Wanasiasa wa upinzani wameonya uwezekano wa kutokea ghasia iwapo uchaguzi huo hautafanyika kwa kuzingatia mfumo ambao utakubaliwa.

Mfumo utakaotumika kumchagua rais

Baada ya miezi kadhaa ya kutokubaliana kuhusu mfumo wa kutumia katika uchaguzi huo, serikali kuu na viongozi wa.

shirikisho walikubaliana kuandaa uchaguzi usio wa moja kwa moja kuwachagua wabunge na rais.

Katika mfumo huo, wajumbe kutoka kila ukoo wanachagua wabunge halafu wabunge hao wanamchagua rais.

Imekubaliwa kwamba wanachama kutoka katika majimbo wataunda kamati ambayo itashughulikia migogoro baada ya uchaguzi ndio katika ngazi za kanda.

Abdishakur amesema kwamba serikali imeidhinisha majina ya wanachama wanaopendelea utawala wa sasa mjini Mogadishu na katika maeneo mengine.

"wameteua watu kutoka shirika la usalama wa taifa NISA, watu kutoka kwa ofisi yar ais, waziri mkuu na ofisi nyingine za serikali. Sheria inasema kwamba watu wanaohusika katika kusimamia uchaguzi wanastahili kuwa watu wasiokuwa na upendeleo wowote na sio kutoka mashirika ya usalama, na wawe ambao raia wanaamini kwamba hawana upendeleo wowote.”

Maafisa wa uchaguzi watakiwa kuajibika

Licha ya ukosoaji huo, serikali ya Somalia inaendelea na mipango ya kuandaa uchaguzi wa bunge na urais unaotarajiwa kufanyika kabla ya Februari tarehe 8.

Naibu wa waziri mkuu wa Somalia Mahdi Gulaid amewataka maafisa wa uchaguzi kufanya kazi yao kulingana na sheria.

Amesema "mnastahili kuaminika, kuwajibika na kutopendelea upande wowote. Mnastahili kuongozwa kulingana na sheria za uchaguzi ili haki ipatikane katika shughuli nzima ya uchaguzi. Hamstahili kuwa na upendeleo na kumnyima mshindi haki yake."

Uchaguzi wa Somalia wa mwaka 2016 uligubikwa na shutuma za hongo na wizi.

Rais Farmaajo, ambaye alishinda uchaguzi huo, anagombea mhula mwingine.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG