Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:52

Somalia yaahirisha tena uchaguzi


Raia wa Somalia
Raia wa Somalia

Kwa mara nyingine, Somalia imeahirisha uchaguzi wa bunge la chini, hadi tarehe 31 mwezi huu wa Machi, mchakato ambao tayari umechelewa kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha mvutano mkubwa wa kisiasa.

Kamati ya uchaguzi ilitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo jana jioni, hatua ambayo, pia utachelewesha zaidi uchaguzi wa rais mpya na kuendeleza mzozo wa kisiasa katika nchi ambayo pia inakabiliwa na changamoto za ukame na waasi wa Kiislamu.

Baada ya kucheleweshwa mara kadhaa hapo awali, uchaguzi wa baraza la chini, ulipaswa kukamilika tarehe 15 mwezi Machi mwaka huu.

Lakini ni majimbo matatu tu kati ya matano ya Somalia yalikuwa yamechagua wawakilishi wao kwa muda uliopangwa, kulingana na maafisa wa uchaguzi.

Viti 39 kati ya 275 vilisalia bila kujazwa katika majimbo ya Hirshabelle, Jubaland na Puntland, kwa mujibu wa Shirka la habari la AFP.

Tume ya uchaguzi ilisema nafasi hizo zitajazwa mwishoni mwa mwezi na "matokeo rasmi ya mwisho" kutangazwa tarehe 31 mwezi huu.

"Wawakilishi wote waliochaguliwa wataapishwa mjini Mogadishu Aprili 14," kamati ya uchaguzi ilisema katika ratiba yake iliyosahihishwa hivi karibuni.

Uchaguzi wa wabunge wa ngazi ya chini na ya juu ulipaswa kukamilishwa kabla ya muhula wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kukamilika Februari 2021.

Malumbano ya kisiasa yamezuia mchakato huo, na mamlaka ya rais yalimalizika kabla ya uchaguzi huo kufanyika.

XS
SM
MD
LG