Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 14:36

Maafisa wa polisi Somalia wakamatwa kwa kuwatesa waandishi


VOA Somali Journalist Released From Puntland Prison
VOA Somali Journalist Released From Puntland Prison

Serikali ya Somalia imesema maafisa wa polisi wanaoshutumiwa kuwatesa waandishi wa habari waliokuwa wanaandika habari kuhusu mashambulizi ya al-Shabaab mjini Mogadishu, wamekamatwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani Abdullahi Nur amesema kwamba maafisa hao wa usalama watawajibika kwa vitendo vyao.

Televisheni inayomilikiwa na serikali imeandika ujumbe wa tweeter wenye picha ya waandishi wa habari wakiwa wamelala chini huku wamefunikwa nyuso zao.

Maafisa wa polisi waliwalenga waandishi wa habari wanaofanya kazi na vituo binafasi vya televisheni ndani ya Somalia, waliokuwa wanafuatilia mashambulizi ya wapiganaji hao dhidi ya vituo vya polisi, Jumanne.

XS
SM
MD
LG