Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:52

Wanamgambo wa al-Shabaab washambulia Mogadishu


Mtoto akivuka eneo la ukaguzi la kituo cha polisi lililoshambuliwa na al-Shabaab nje ya mji wa Mogadishu, Somalia Jumatano, Feb. 16, 2022. (AP Photo/Farah Abdi Warsameh)
Mtoto akivuka eneo la ukaguzi la kituo cha polisi lililoshambuliwa na al-Shabaab nje ya mji wa Mogadishu, Somalia Jumatano, Feb. 16, 2022. (AP Photo/Farah Abdi Warsameh)

Wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia vituo vya polisi na maeneo ya ukaguzi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu mapema asubuhi ya leo, maafisa wamesema.

Taarifa zinasema kulisikika milio mikubwa ya bunduki na milipuko.

Hata hivyo waziri wa usalama wa ndani Abdullahi Nor aliandika katika mtandao wa Twitter kwamba vikosi vya usalama vimewashinda wanamgambo wanaojihusisha na al-Qaida.

Hakuna taarifa za haraka zilizotolewa kuhusiana na majeruhi au vifo.

Wiki iliyopita takriban watu sita walikufa na wengine kadhaa walijeruhiwa baada ya shambulizi la kujitoa muhanga kulenga basi dogo lililokuwa limejaa wajumbe wanaojihusisha na uchaguzi wa bunge unaondelea nchini.

XS
SM
MD
LG