Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:49

Magufuli aomboleza kifo cha Sir George Kahama


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Sir George Kahama amefariki dunia Jumapili akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Rais John Magufuli ametuma rambirambi zake kwa familia ya marehemu akisema taifa limepoteza mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru, maendeleo na ustawi wa jamii ya watanzania.

Pamoja na familia ya marehemu, Dkt Magufuli amewapa pole nyingi wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi, wabunge, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huo.

Rais Magufuli amesema katika salamu hizo: "Sir George Kahama alikuwa kiongozi shupavu, mzalendo, mwanasiasa mahiri, aliyewapenda watanzania na aliyejitoa kushirikiana na viongozi wenzake akiwemo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kupigania uhuru, kujenga misingi ya Taifa likiwemo Azimio la Arusha, kujenga misingi ya uchumi wa ujamaa na kujetegemea na mengine mengi, kwa hakika hatutamsahau"

"Japo kuwa Sir George Kahama ametangulia mbele za haki, sisi viongozi tuliopo tutamuenzi kwa kuhakikisha tunaendeleza juhudi za kuipigania Tanzania aliyoshiriki kuijenga, na pia tunamuombea kwa Mnyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.

XS
SM
MD
LG