Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 05:23

CCM yajivua 'gamba,' kufanya mabadiliko


Mwenyekiti wa CCM John Magufuli
Mwenyekiti wa CCM John Magufuli

Mkutano mkuu maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umepitisha mabadiliko ya katiba ya chama hicho yenye lengo la kuboresha na kufanya marekebisho ya mfumo wa chama kwa manufaa ya wananchi na wanachama kwa ujumla.

Mabadiliko hayo yakiwa ni ya 16 kutokea ndani ya chama hicho cha ccm tangu kuanzishwa kwake yalipitishwa na jopo la wajumbe wa mkutano Mkuu maalum zaidi 2000 ambao ni sawa na asilima 96 ya wajumbe wote.

Akizungumza katika mkutano huo mjini Dodoma Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema mabadiliko hayo yanalenga kurudisha ufanisi, heshima na utendaji makini wa CCM uliokuwa umeshuka kiwango.

Hilo amesema limetokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho kutokuwa na weledi na moyo wa kukitumikia Chama hicho na wananchi.

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa mabadiliko ya katiba ndani ya chama hicho pia yatajikita katika kuhakikisha vyeo visivyo na tija kwa chama hicho na ambavyo havimjo ndani ya katiba ya CCM vinaondolewa.

Pia ametaka sambamba na hilo chama kipunguze wingi wa vikao vilivyokuwa vikifanyika mara kwa mara hapo awali badala yake Chama hicho kijikite zaidi katika kushughulikia na kutatua kero za wananchi badala ya kufanya vikao visivyo na tija.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo amesema CCM inazidi kuimarika katika maeneo mengi nchini huku imani ya wananchi kwa Chama hicho ikizidi kuongezeka kwa kasi huku pia akielezea namna ambavyo Serikali ya awamu ya tano inavyozidi kutekeleza ilani ya Chama hicho kwa vitendo.

Hilo limeweza kufanikiwa tangu ilipoingia madarakani na kutaja mafanikio mbalimbali yaliyotokana na utendaji kazi madhubuti wa Serikali hiyo ikiwemo udhibiti wa matumizi mabaya wa fedha za umma pamoja na ongezeko la ukusanyaji mapato

Kwa upande wao Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wamesifu mabadiliko hayo na kusema yataleta tija kwa Chama hicho ikiwa pamoja na kuwatumikia vyema wananchi huku wakisisitiza kuendelea kwa chama kushughulikia usaliti ndani ya chama hicho.

XS
SM
MD
LG