Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 19, 2022 Local time: 13:52

CCM yamfukuza uanachama Sophia Simba


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi John Magufuli

Chama cha Mapinduzi katika mkutano wake mkuu unaoendelea Dodoma, Tanzania, Jumamosi kimemfukuza mwanachama wake mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba.

Wakati huo huo chama kimetoa msamaha kwa Adam Kimbisa na kimempa onyo kali Emmanuel Nchimbi wote ni wanachama wa CCM. Imeelezwa kuwa onyo kali alilopewa Nchimbi lina maana ya kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa kipindi cha miaka minne.

Katika taarifa hizo za Chama Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida amefukuzwa pia. Wenyeviti wengine ni Jesca Msambatavangu (Iringa), Erasto Kwilasa (Shinyanga) na Christopher Sanya (Mara). Pia Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kigoma Josephine Genzabuke amepewa onyo kali.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika.

Kwa hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.

Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga Ernest Kwirasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Nesta Msabatavunga, Mjumbe wa Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.

Wengine zaidi ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido Leiza amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Molleli, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Hawadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC Gureta.

Taarifa hizo za chama zimeeleza kuwa waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye amepewa onyo kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha, Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC Tunduru, Cheif Kalolo ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Dina Chahali, Tanzania

XS
SM
MD
LG